MUONEKANO KUCHA ZAKO NA AFYA YA MWILI.

Kucha ni nini ?

Ukucha au kucha ni sehemu ya mwili wa wanyama ikiwemo jamii ya sokwe na wanadamu ambayo inapatikana kwenye vidole vya miguu na mikono. Kucha zimekua na kazi mbali mbali kulingana na zama husika; kwa mfano kipindi cha zama za kale kama ujima na zinginezo, kucha zimekua zikisaidia kwenye kujilihami pale mnyama anapokua amevamiwa na mnyama mwingine. Lakini pia, kucha imekua imekua ni moja ya sehemu ya mwili zinazopenedezesha mwili na kwenye kuandaa chakula.

 Katika upande wa elimu ya Afya na Utabibu, kucha zimekua na kazi nyingi sana lakini katika hizo kazi, moja wapo ni kutoa kiashiria cha usalama wa mwiliWatu wengi wamekua namaswali mengi juu ya muonekano wa kucha zao. kuwepo kwa alama kama madoa tofauti katika kucha n kitu cha kawaida lakini zipo alama kadhaa kuwepo kwake kwenye ukucha huwa ni ishara ya uwepo wa maradhi au tatizo fulani mwilini. 


                   Chanzo cha Picha: Jambo Times


Alama zinazoashiria uwepo wa matizo mwilini

Mkanda mweupe kwenye ukucha (Muehrcke's Nails)

Kuwepo kwa mikanda yenye rangi nyeupe kwenye ukucha kama inavyonekana hapo chini ni ishara ya kuwepo kwa tatizo linalohusiana na ini na Figo, lakini pia wagonjwa walioko kwenye matibabu ya saratani kwa kutumia madawa. Hivyo ukiona ukucha wako uko na hiyo hali basi fika katika kituo cha kutolea huduma za Afya kinachotambulika na serikali.

 

                Chanzo cha Picha: B M J Case Reports

Kucha zilizotengeneza mgongo (Clubbing nails)

Kama ukucha wako umebadilika muonekano na kuwa na muonekano wa kutuna au kuwa na mgongo kama inavyoonekana hapo chini, ni ishara ya kuwepo kwa tatizo katika moja viungo vifuatavyo; Ini, figo, Mapafu, Moyo na Shambulio kwenye utumbo mpana (Inflammatory Bowel Disease) na mambukizi ya Virusi vya ukimwi (VVU).

 

           Chanzo cha Picha: eMedicine Health

 

Mistari ya mbonyeo kwenye ukucha (Beau's lines)

Kuwepo kwa mbonyeo kwenye kucha ambao unakua kama vile yalivyo matuta huku yakiwa na rangi ya damu kwa mbali ni ishara ya kuwepo kwa jeraha kwenye kucha na kusababisha kuvujia kwa damu. Mbali na hilo uwepo kwa hali hiyo kumekua kukihusishwa na kuwepo kwa matatizo katika; Mishipa ya damu ya pembeni (peripheral vascular system), Kisukari na upungufu wa Madini ya zinki (Zn)

           Chanzo cha Picha ni B M J Case Reports

Kucha kuwa na bonde kama kijiko (koilonychia)

Ukucha unapobadilika muonekano na kua kama kijiko, kama ilivyoonekana hapo chini ni ishara ya kuwepo kwa tatizo kwenye mfumo wa damu au kuumia kwa kujirudia au kukutana na kemikali zinazoathiri ukuaji wa kucha. Katika mfumo wa damu, mwili unapokuwa umepungukiwa na madini chuma (Iron, Fe) kupita kiasi (severely) moja ya vitu ambavyo  hubadilika ni ukucha. kama inavyonekana hapo chini.

 

                                            
            Chanzo cha Picha ni Healthline

 

Kucha kuwa kama Sahani nyeupe (Terry's nails)

Muonekano wa kucha kama sahani nyeupe na kuwa na mkanda rangi ya damu ya mzee au nyeusi wakati fulani kenye ncha ni ishara ya kuwepo kwa tatizo kama vile Kisukari, Ugonjwa wa moyo (CHF) na mambukizi ya virusi vya ukimwi (HIV). Wagonjwa wengi waliopatikana na matatizo ya ini mara nyingi huwa na aina aina hiyo ya muonekano wa kucha.

            Chanzo cha Picha; American Journal of Medicine

 

Kucha kuvunjika vunjika kiuwa za njano na kuvunjika

Kama ilivyoelezwa hapo juu, kucha zinazokazi nyingi ikiwemo kudhirisha maradhi au matatizo yaliyopo kwwnye mwili. Kucha kuwa za njano na kuvunjika mara kwa mara ni ishara ya kuwemo kwa maambukizi ya vimelea kuvu (fangasi). Wadudu kuvu (fangasi) mara nyingi hutokea kwa sababu kutokujua namna nzuri ya kuzitunza na kuzihudumia kucha na kugusa maji maji mara kwa mara. Hii hali hutokana na kuwepo kwa unyevu unyevu muda mwingi ambako hutokana na kujishughulisha na shughuli zinazohusisha maji kwa mfano udobi na zingine zinazohusiana na hizi. 


                   Chanzo cha Picha; Springer Link


Kama unataka kujua namna gani ya kuzuia kucha zako zisipoteze muonekano au zisikatike katike ovyo, bonyeza Hapa. Hata hivyo, kama dalili hizo zitaonekana kwenye kucha zako fika kituo cha kutolea huduma za Afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu. 





Comments