ZIFAHAMU DAWA ZA MAUMIVU
SALAMA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO.
Habari za wakati tena mpenzi msomaji wa blogi yako ya
“ZIJUE DAWA ZAKO” ambayo kila siku inakuletea elimu mpya inayohusu dawa za binadamu. Mfamasia wako hewani leo ninataka kukupatia ufahamu juu ya dawa zinazotumika kupoza maumivu kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.
Labda kidogo nigusie kuhusu vidonda vya tumbo.
Mfumo mzima wa njia ya chakula ambayo kwa kitaalamu unaitwa
“GASTROINTESTINAL SYSTEM”, mfumo huu wa chakula unafanya kazi kadha wa kadha.
Baadhi ya kazi za mfumo wa chakula ni pamoja na;
Ø Kumeng’enya chakula
Ø Kutoa mabaki ya chakula nje ya mwili
Ø Kufyonza maji na chumvi chumvi muhimu kwajili ya shughuli za kimwili
Ø Kufyonza virutubisho vilivyomo kwenye vyakula n.k
Vidonda vya tumbo husababishwa na vitu wa kadha kadha , Lakini hadi sasa tafiti za kitabibu zinaoneysha kuwa visababishi vya vidonda vya tumbo ni kama vifutavyo;
- Matumizi ya dawa za kutuliza maumivu zilizopo kwenye kundi la NSAIDS, kwa muda mrefu.
- Kuwa na maambukizi ya mdudu aitwaye Helicobater pylori.
- Msongo wa mawazo (stressi)
- Uvutaji wa sigara
Mada yetu leo kama nilivyo tangulia kuandika kwenye kichwa
cha habari, Dawa za maumivu ambazo si salama kwa mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo. Dawa hizi ambazo tutakazo zijadili leo zile ambazo zinatumika kupoza maumivu kwa mgonjwa mwenye;
v Historia ya vidonda vya tumbo na anasumbuliwa na maumivu sehemu yoyote ya mwili.
v Maumivu yanayotokana na vidonda vya tumbo.
Maumivu sehemu yoyote ya mwili inahusisha maumivu ya kichwa,
miguu na sehemu zingine za mwili. Kwa mgonjwa mwenye maumivu hayan a pia anahistoria ya kuwa na vidonda kwenye mfumo mzima wa utumbo wa chakula anapaswa kuwa natahadhari sana anapotaka kutumia dawa za maumivu.
Katika dawa za maumivu ya tumbo, lipo kundi la
dawa ambalo hutumika mara nyingi katika kupoza maumivu. Kundi hili kitaalamu linaitwa
“NON-STEROID ANTI-INFLAMMATORY DRUGS” au kifupi “NSAIDS”. Kulingana na tafiti na maandiko mbalimbali ya kitabibu,
Dawa ambazo ziko katika kundi hili zimekuwa zikisababisha vidonda vya tumbo ama michubuko kwenye mfumo wa chakula. Hivyo basi kama wewe unavidonda vya tumbo au ulishawahi kuwa na vidonda kipindi cha
nyuma, dawa hizi zinaweza kufanya hali ya vidonda vyako kuwa mbaya zaidi nakusababisha maumivu makali badala ya kukusaidia kupoza maumivu uliyonayo.
Hivyo basi kabla ya kutumia dawa za maumivu zozote ulizopatiwa na mtoa huduma za afya,
inashauriwa ni vyema sana kumpatia taarifa daktari
au mfamasia anayekuhudumia kwamba ulishawahi kuwa na vidonda vya tumbo
au unavidonda vya tumbo. Taarifa unazompatia zinamsaidia yeye kukupatia dawa ambazo hazisababishi vidonda vya tumbo.
Katika kundi hili la dawa ziitwazo “NSAIDS”
ambazo si salama kwa mgonjwa na mtu aliye na historia ya vidonda vya tumbo,
baadhi ya dawa zinazopatikana katika kundi hili ni pamoja na;
- Aspirin
- Diclofenac
- Ibuprofen
- Meloxicam
- Indomethacin
- Aceclofenac
- Celecoxib
- Naproxen
- Piroxicam
- Etodolac
- Ketoprofen
- Fenoprofen
Dawa hapo juu ni baadhi ya dawa zilizopo katika kundi hili liitwalo
“NSAIDS”.
Sasa hebu tuone ni dawa zipi zafaa kutumia kwajili ya kutuliza maumivu kwa mtu aliye navidonda vya tumbo na
pia anahistoria ya vidonda vya tumbo.
1.
Maginisiamu (Magnisium Hydroxide) na Alluminium
(Aluminium Hydroxide).
Natumaini majina haya sio mapya machoni pako, hizi dawa zinapatika na hata kwenye maduka ya dawa muhimu ambayo hata hapo mtaani kwako yanaweza kuwepo.
Dawa hizi zinasaidia sana kupoza maumivu makali ya tumbo ambayo yanatokana navidonda vya tumbo.
Jinsi ambavyo hizi dawa zinavyopunguza maumivu ya tumbo nikupitia uwezo wake wakupunguza kiasi cha tindikali inayozalishwa na tumbo ambayo inapogusa kuta za tumbo lenye vidonda husababisha maumivu.
Lakini pia dawa hizi zinatakiwa kutumika kulingana na kiasi kinachoshauriwa na mfamasia
au daktari wako anayekuhudumia.
Moja ya madhara ya kutumia kiasi kikubwa cha maginisiamu kwa wakati mmoja ni pamoja na Kusababisha mharisho, Aluminiamu husababisha choo kuwa kigumu lakini pia
inapotumika kwa muda mrefu inaongeza hatari ya kupata magonjwa ya nayosababishwa na vijidudu hatarishi viishivyo kwenye mfumo wa chakula.
2.
Tramado (Tramadol)
Dawa hii inauwezo wa kupoza maumivu bila kuasili hali ya vidonda vya tumbo alivyonavyo mgonjwa.
Lakini pia zipotahadhari kadha za kuzingatia unapotumia dawa hizi.
Moja ya tahadhari nipamoja na;
o
Usitumie kiasi kikubwa cha
dawa kwa wakati mmoja, tumia kiasi cha dawa kama ulivyoelekezwa na mfamasia au
daktari wako. Moja ya madhara yanayotokana na kutumia kiasi kikubwa ni pamoja na choo kuwa kigumu, kusababisha kichefuchefu na hata kutapika.
o
Lakini pia
usitumie dawa hizi bila maelekezo ya mfamasia aliyekupatia dawa hizi
Hyoscine Butyl bromide.
Hii dawa ipo katika kundi la dawa ambazo kitaalamu zinajulikana kama Antispasmodic agent ambayo kazi yake kuu ni kuzuia mikunjo au kujikunja kunja kwa Mfumbo wa Mmeng’enyo wa Chakula yaani kitaalam inajulikana kama Gastrointestinal tract. Hivyo basi dawa hizi pia zafaa pia kwa mtu anayesumbuliwa na Chango hasa hasa wakati wa siku zake (Period)
Basi hadi kufikia hapo utakuwa umeelewa ni dawa zipi zinafaa kutumika kupunguza maumivu kwa mtu aliyenavidonda vya tumbo.
Usisahau kutuandikia maoni yako hapo chini,
tungependa kusikia kutoka kwako.
Comments