Ukucha umeundwa na nini ?
Kucha ni moja ya vipande vya mwili vinavyopatikana sehemu ya juu ya ngozi (japo sio shememu ya ngozi) ambayo ni mikononi na miguuni. Ukucha umetengenezwa kwa protini ijulikanayo kama keratini ngumu. Keratini ngumu ndio hufanya ukucha uwe na hiyo hali ya ugumu ukilinganisha na ngozi au unywele.
Usichokijua ni kwamba kucha hukua kila siku kwa wastani wa urefu wa nusu milimita (0.5mm) hadi milimita moja na nukta tatu (1.3mm) kila siku huku kucha za mikoni zikiwa na ukuaji wa haraka kuliko za miguuni.. Na ukuaji wake huendelea kuwa sawa, hakuna muda utapungua labda kama kutakua na maradhi yanayoshambulia kwenye mzizi (nail root).
Mambo ya kufanya ili kwa na kucha zenye Afya
Kula mlo uliokamili.
Sio kwa ajili ya kucha tu, Ulaji wa mlo uliokamilika (Balanced diet) hauepukiki kwa mtu yoyote anayetaka kuwa na Afya njema. Kucha ni kiungo ambacho pia hutengenezwa kwa kutumia virutubisho vile vile ambavyo sehemu zingine za mwili huhitaji ili kutengeneza chembechembe hai mpya za mwili. Protini ni mojawapo wa kirutubisho kinachohitajika kwa sehemu kubwa ili kutengeneza kucha.
Chanzo cha Picha; Narayana Health
Using’ate au kukata kucha kwa meno.
Kupunguza urefu wa kucha kwa kuzing’ata inaweza isiwe njia salama kwa muhusika kwa meno hayawezi kukata kucha kiusahihi na wakati mwingine husababisha majeraha kwenye sehemu zingine za kucha kupelekea kuingia kwa vimelea vya magonjwa na kusababisha magonjwa kwenye kidole chenye ukucha husika.
Hakikisha zinakua na unyevu nyevu.
Katika shughuli zako za kila siku usiruhusu kucha zako kubaki kavu muda mrefu, hakikisha unazipatia unyevunyevu mara kwa mara kwa kupakaa mafuta maalum kwa ajili ya kucha au mafuta utumiayo kupakaa ngozi yako. Huenda ukawaza kuwa utahitaji kuwa na pesa sana kuzifanya kucha zako ziwe na unyevu unyevu muda mwingi, hapana, waweza kutumia mafuta yaliyo na Glycerin au mafuta ya kawaida yaitwayo vasselin na kucha pamoja na vidole vyako vikawa na unyevunyezu wa kutosha.
Ondoa uchafu kwenye kucha.
Kuwa na kucha chafu si tu kwamba ni hatari kwa kucha zako bali hata kwa Afya ya Mwili pia kiujumla. Kucha ndefu na chafu hutunza uchafu amabo unaweza kuwa umebebelea vimelea vya magonjwa mabali mbali kama vile amiba na kipindu pindu. Hivyo basi ili kuepuka magonjwa yanayoweza kushambulia kucha zako, hakikisha unaondoa uchafu kwenye kucha zako mara kwa mara.
Usiguse maji mara kwa mara.
Katika shughuli za kila siku, huenda hakuna siku inayokwisha bila mikono kukutana na maji na inaweza kuwa ni kwa sababu tulikua tunanawa, tunasafisha vifaa vya nyumbani, kufua, kuoga na zingine nyingi za kufanana na hiyo. Pamoja na kwamba ni nyingi sana mikono yetu inakutana maji, hatutakiwi kuruhusu mikono yetu kuwa imelowana maji kila mara kwani kitendo hiki hupelekea kudhoofu kwa misingi ambako ukucha huanzia. Nini ufanye kama wewe ni mtu unagusa maji karibia masaa yote ya siku ? Jibu ni kwamba, hakikisha mikono inakakaushwa mara kwa mara kwa kutumia kitambaa safi au Karatasi laini (tishu) ili kuepuka kucha kudhoofu na kupoteza muonekano wa kuvutia.
Ng’arisha kucha zako.
Usafishaji wa kucha unaweza kuwa chanzo cha majeraha kwenye kucha au kidole cha muhusika kama tu zoezi zima la kusafishia kucha linafanyika ndivyo sivyo au kutumia vifaa visivyo sahihi. Utumiaji wa vifaa visivyosahihi kung’arisha kucha inaweza kuwa hatari kwa Afya kucha zako, kwa mfano; kutumia mawe, nyembe, visu na mikasi kung’arishia kucha. Nenda kwenye maduka ya urembo nunua kifaa maalum kwa ajili ya kusafishia au kung’arishia kucha.
Huduma ya kuimarisha kucha.
Tumia mafuta yatakanayo na mimea, yajulikanayo kama vegetal na essential oils, itakua vyema kama utapata mafuta yaliyoandaliwa tayari kwa ajili ya kudondoshea kwenye kucha na kwa ajili ya kuzifanya kucha zako ziwe na unyevu nyevu muda mwingi.
Tumia Kirutubisho vya kuimarisha kucha (Biotin).
Virutubisho vingine vilivyotajwa hapo juu zinao mchango mkubwa kwenye kuwa na kucha zilizo na Afya. Tafiti nyingi zilizofanywa hivi karibuni zimeonyesha kuwa, Matumimizi ya vitamin H (Biotin) kama kirutubisho cha ziada (supplement) imekua ni kichocheo kikubwa kwa ukuaji na Afya nzuri za kucha. Hivyo, kama utahitaji kucha zikue kwa afya nzuri unaweza ongeza hicho kirutubisho au chakula chenye kirutubisho kwenye matumizi yako ya kila siku.
Chanzo cha Picha; alamy
Pakaa kucha rangi.
Kupakaa kucha rangi pia kumekua na mchango kwenye Afya na ukuaji wa kucha za sehemu zote, miguuni na mikononi. Upakaji rangi unaofuatana na migongo ya kucha na sio tofauti, tizama picha hapo chini. Rangi za kucha zinazosalama kwa Afya ya kucha ni pamoja na rangi zenye uwezo wa kupitisha mwanga (transparent gel). Rangi zenye muonekano huu husaidia sana kucha kukua na kuimarika.
Chanco cha Picha; OnlySky
Pumzisha kucha zako
Upakaji kucha rangi mfululizo bila kuzipumzisha ni hatari kwa Afya. Kupaka rangi unaweza usiwe na madhara tu kama unazipa pumziko kucha zako, kila unapopakaa kucha mara tatu au mara mbili basi pumzisha kucha zako na rangi, ziache angalau wiki moja au mbili bila kuzipaka rangi. Hii itazifanya kucha zako ziwe na Afya na muonekano mzuri.
Tahadhari; Usitumie bidhaa zilizotajwa kwenye ukurasa huu bila kupata maelekezo yaliyosahihi kutoka kwa watoa huduma za Afya, mfamasia au Daktari wa Ngozi.
Comments