Mfamasia ni nani ??
Mfamasia ni mtaalamu wa Afya aliyebobea kwenye mambo ya dawa za Binadamu, kwenye masuala ya dawa mfamasia ndiye mtu ambaye anayajua mambo mengi kuhusu usalama, utendaji ufanisi na ubora wa dawa zako.
Mfamasia kwa lugha ya kingereza anafahamika kwa majina mengi kama ambayo ilivyoorodheshwa hapa chini;
- Pharmacist
- Druggist
- Dispensing Chemist
- Apothecary
- Pharmaceutist
Mfamasia ni moja kati ya wanatimu katika kundi la watoa huduma za Afya, katika kundi hili la watoa huduma za afya, mfamasia hufanya mambo yafuatayo;
- Kuhakikisha mgonjwa anapata dawa zilizo na ubora
- Kuhakikisha utoaji wa dawa za binadamu unafuata sheria na kanuni zilizopo
- Kuhakiki kama dawa anazopata mgonjwa zinamfaa mgonjwa husika.
- Wajibu mwingine wa mfamasia ni kutoa maelekezo jinsi dawa zinavyopaswa kunywewa/kutumika na pia kumsaidia au kujibu maswali ya mgonjwa juu ya dawa.
Majukumu mengine ya mfamasia ni pamoja na;
- Kusimamia mrorongo mzima wa upatikanaji wa dawa kutoka inapotengenezwa hadi inapomfikia mteja au mgonjwa na kuhakikisha pia maeneo ambapo shughuli za uuzaji wa dawa (famasi) na mifumo inayotuma pale inafaa kwajili ya shughuli nzima.
- Kutoa ushauri kwa watoa huduma za afya wengine juu ya Matumizi, Usalama na Ufanisi wa dawa na pia kupendekeza mifumo sahihi ya utoaji wa huduma za dawa za Binadamu.
- Kushiriki katika utoaji elimu kwa jamii kama umuhimu wa kuacha kuvuta sigara na kuacha kunywa pombe.
Je, ni maeneo gani ambapo mfamasia anaweza kufanya kazi tofauti na hospitalini ?
Maeneo ambayo mfamasia anaweza kufanya kazi ni pamoja na;
- Kwenye maduka ya dawa yanazohudumia jamii (community pharmacy), maduka haya yanaweza kuwa jumla jumla ama reja reja.
- Uzalishaji wa madawa viwandani akiwa kama msimamizi wa zoezi zima la uzalishaji na utengenezaji wa nadawa kiwandani hapo.
- Na sehemu zingine nyingi kama magerezani, taasisi za kitafiti, maduka ya dawa za mifugo na kwenye taasisi za elimu kama mkufunzi.
Mfamasia huyu hawezi kuanza kufanya kazi kama hajasajiliwa na baraza la famasi nchini, hivyo wafamasia wote hupaswa kukizi vigezo muhimu vya kusajiliwa na kupewa leseni ya kutumikia umma.
Chanzo cha Picha hii |
Comments
mimi James kutoka katavi
Kusomea fani ya famasi katika ngazi ya Diploma inahitajika uwe umefaulu masomo yafuatayo ;
Chemistry -uwe umefaulu kuanzia Alama D au zaidi
Biology - uwe umefaulu kuanzia Alama D au zaidi
Pia uwe umefaulu masomo mengine mawili yasiyo ya Dini kwa ufaulu kuanzia Alama D au zaidi.
Kuhusu swali lako la kuhusu medically sijalielewa unaweza kufafanua zaidi ndugu ili niweze kukujibu kwa ufasaha.
2.mtu km hajasom kbsa pharmacy na anatka kumilik DLM utarabib unakuwa vipi