MFAMASIA NI NANI ?

Mfamasia ni nani ??

Mfamasia ni mtaalamu wa Afya aliyebobea kwenye mambo ya dawa za Binadamu, kwenye masuala ya dawa mfamasia ndiye mtu ambaye anayajua mambo mengi kuhusu usalama, utendaji ufanisi na ubora wa dawa zako.
 Mfamasia kwa lugha ya kingereza anafahamika kwa majina mengi kama ambayo ilivyoorodheshwa hapa chini; 

  • Pharmacist
  • Druggist
  • Dispensing Chemist
  • Apothecary
  • Pharmaceutist
 Mfamasia ni moja kati ya wanatimu katika kundi la watoa huduma za Afya, katika kundi hili la watoa huduma za afya, mfamasia hufanya mambo yafuatayo;
  • Kuhakikisha mgonjwa anapata dawa zilizo na ubora
  • Kuhakikisha utoaji wa dawa za binadamu unafuata sheria na kanuni zilizopo
  • Kuhakiki kama dawa anazopata mgonjwa zinamfaa mgonjwa husika.
  • Wajibu mwingine wa mfamasia ni kutoa maelekezo jinsi dawa zinavyopaswa kunywewa/kutumika na pia kumsaidia au kujibu maswali ya mgonjwa juu ya dawa.

Majukumu mengine ya mfamasia ni pamoja na;
  •  Kusimamia mrorongo mzima wa upatikanaji wa dawa kutoka inapotengenezwa hadi inapomfikia mteja au mgonjwa na kuhakikisha pia maeneo ambapo shughuli za uuzaji wa dawa (famasi) na mifumo inayotuma pale inafaa kwajili ya shughuli nzima.
  • Kutoa ushauri kwa watoa huduma za afya wengine juu ya Matumizi, Usalama na Ufanisi wa dawa na pia kupendekeza mifumo sahihi ya utoaji wa huduma za dawa za Binadamu.
  • Kushiriki katika utoaji elimu kwa jamii kama umuhimu wa kuacha kuvuta sigara na kuacha kunywa pombe.


Je, ni maeneo gani ambapo mfamasia anaweza kufanya kazi tofauti na hospitalini ?
 Maeneo ambayo mfamasia anaweza kufanya kazi ni pamoja na;

  • Kwenye maduka ya dawa yanazohudumia jamii (community pharmacy), maduka haya yanaweza kuwa jumla jumla ama reja reja.
  • Uzalishaji wa madawa viwandani akiwa kama msimamizi wa zoezi zima la uzalishaji na utengenezaji wa nadawa kiwandani hapo.
  • Na sehemu zingine nyingi kama magerezani, taasisi za kitafiti, maduka ya dawa za mifugo na kwenye taasisi za elimu kama mkufunzi.
Mfamasia huyu hawezi kuanza kufanya kazi kama hajasajiliwa na baraza la famasi nchini, hivyo wafamasia wote hupaswa kukizi vigezo muhimu vya kusajiliwa na kupewa leseni ya kutumikia umma.

Chanzo cha Picha hii











Comments

Karibuni sana kwa maswali
Unknown said…
nilikua nauliza mfamasia anasoma madawa ya mifugo au!!!!!?
Hapana ndugu, kama nilivyoandika kwenye post zangu. Mfamasia ni mbobezi katika elimu ya madawa yanatumika kutibu magonjwa ya binadamu.
Unknown said…
ukitaka kusomea madawa kwa maana ya mfamsia ngazi ya diploma vigezo vinakuwa je na n nn majukumu ya ziada tofauti na medically hasa ktk kipindi hiki ambacho hakuna ajira
mimi James kutoka katavi
Unknown said…
Coz ya pharmacy inachukua muda gani ??
Habari James
Kusomea fani ya famasi katika ngazi ya Diploma inahitajika uwe umefaulu masomo yafuatayo ;
Chemistry -uwe umefaulu kuanzia Alama D au zaidi
Biology - uwe umefaulu kuanzia Alama D au zaidi
Pia uwe umefaulu masomo mengine mawili yasiyo ya Dini kwa ufaulu kuanzia Alama D au zaidi.
Kuhusu swali lako la kuhusu medically sijalielewa unaweza kufafanua zaidi ndugu ili niweze kukujibu kwa ufasaha.
Inachukua muda gani kufanya nini ?? Fafanua zaidi ndugu
Unknown said…
Mtu akisoma pharmacy mwak mmja au miwili anapta kibali ya kutowa dawa.
2.mtu km hajasom kbsa pharmacy na anatka kumilik DLM utarabib unakuwa vipi
Unknown said…
Kama nina d ya biology na d ya kemia alafu math nimepata f naweza kusoma
Anonymous said…
Nahitaj mfamasiy kwenye Duka lang l rerj rej no 0626895762