Je, waijua njia rahisi ya Kutengeneza sanitizer bila gharama ?

 NAMNA YA KUANDAA HAND SANITIZER NYUMBANI.

Kwanini tunapaswa kunawa mikono?

Vimelea visababishavyo matatizo ya Kiafya kwa binadamu au hata Wanyama vinaweza kupatikana hata katika sehemu tofauti tofauti za mwili wa mwanadamu bila kusahau sehemu zenye majeraha na vidonda. Kwa mujibu wa tafiti za kitabibu, maeneo kama vile maeneo ya ubavuni (kwa kimombo axillary areas), Kwapani, Maeneo ya tumbo la chini karibu na sehemu ambapo mshipa wa ngili hutokea. Si hivyo tu, mikono yetu na sehemu zingine zimekua ni mazalia ya vimelea kama vile S.aureus, Shigella, Proteus mirabilis, vimelea jamii ya Krebsiella ambapo katika Ngozi ya mgonjwa aliyeko wodini anaweza kuwa na vimelea kuanzia 100 hadi milioni moja (1.0 x 10).  Hii ndio sababu unahitaji kunawa mikono yako kila baada ya kugusana na kitu chochote wodini kwani uwezekanao wa kupata maambukizi mapya ni mkubwa kuliko ambavyo mtu wanaweza kudhani.


Yapo mambo ambayo tumezoea na yamekuwa yakifanywa na jamii zetu kama sehemu ya ustarabu au utamaduni wetu ambayo kwa namna moja aua nyingine imechangia kuongezeka kwa au kuenea kwa vimelea hivi, mambo hayo ni Pamoja na Kushikana mikono, kugusana Ngozi kwa Ngozi, kuchangia nguo au matandiko na kukumbatiana. Hivyo ni vyema kupunguza mazoea ya kufanya tabia hizo ili kuzuia maambukizi au kuenea kwa vimelea na hata ugonjwa kutokea.

 Picha. 01 Ni picha inaonyesha vimelea ambavyomtu ambaye ameshika matandiko au kugusa gusa vitu huko wodini. [Chanzo cha Picha ni Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Katika dunia tuishio, magonjwa yamekua ni mengi sana na baadhi ya magonjwa hayo yanaennezwa kwa kugusana kati ya binadamu na binadamu na baadhi ni kugusana binadamu na Wanyama. Katika magonjwa haya yapo yale ambayo huenea kwa kula chakula kichafu au chakula ambacho kina vimelea vinavyo sababisha tumbo kuumwa au hata mwili mzima kuugua. Katika jambo hili ndipo tunapoona umuhimu wa kuosha mikono yetu mara kwa mara wakati tunaandaa chakula na wakati tunapotaka kukitumia chakula hicho. 

Kuosha mikono imekua ni moja ya njia rahisi na nafuu ya kujikinga na maradhi yasabibishwayo na vimelea viishivyo ardhini au sehemu yoyote ambapo binadamu hushika au hugusa mara kwa mara. Tafiti zinaonyesha hivi, Kutumia mililita tatu (3ml) za sabuni ya maji au Kitakasa mikono chenye ethanol au pombe inatosha kabisa kuondoa maelfu ya vimelea kwenye mikono ya mtu. Hivyo ni vyema kutumia kiasi cha kutosha cha sabuni wakati wa kunawa mikono kupunguza au kuondoa vimelea mikononi mwetu.

Je, Kipi bora Zaidi kati ya kunawa mikono na maji tu au Kutumia maji na sabuni au Kitakasa mikono chenye ethanol au pombe.?

Utafiti uliofanywa na Trick na wenzake, utafiti wao ulilinganisha ufanisi wa vitu hivi vitatu kwenye kutakasa mikono; Sabuni ya maji, Kitakasa mikono chenye pombe (62%) na maji tiririka pekee ambapo vitakasa mikono vilivyo na pombe kwa asilimia 62 vimeonyesha kuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko njia hizi tajwa. Hivyo ufahamu kuwa, kunawa ni njia nzuri ya kuondoa vimelea ila sio njia bora, Kitakasa mikono ndio njia bora kabisa kuondoa vimelea mikononi.

 

Namna ya kuandaa kitakasa mikono majumbani. 

Ili kukurahisishia kuelewa namna ya kaundaa kitakasa mikono inabidi tuchague kiasi tunachohitaji kuzalisha, ambapo hapa tunataka tujifunze namna ya kuzaliasha kitakasa mikono chenye ujazo wa lita moja (1L). Katika kuandaa kitakasa mikono kwa kiasi cha lita moja, kuna formula mbili ambazo hutumika kuandaa kitakasa mikono chenye pombe (Alcohol) katika wingi wa asilimia 60 hadi 70. Formula zenyewe ni;

    1. Njia ya kwanza (formulation I). Njia hii hutuwezesha kutengeneza kitakasa mikono kiasi cha Lita moja chenye viambata katika wingi huu; Pombe (Ethanol 80%v/v), Haidrojen peroksaidi 0.125v/v, Glisarini 1.45% v/v. Kiasi na kiwango katika wingi (Percentage concentration) 

  • Kemikali iitwayo Haidrojen peroksaid (H2O2) ya 3%; Hapa utahitajika kuandaa kiasi cha mililita 41.7 za Hydrogen peroxide 3% ambayo hii waweza ipata famasi ambako huzwa katika ujazo wa mililita 100.
  • Pombe au Ethanol yenye 96%; Hapa utahitajika kuandaa kiasi cha mililita 833.3 za pombe yenye asilimia 96 ambayo hii waweza ipata katika maduka yauzayo kemikali za maabara.
  • Kemikali iitwayo Glycerol yenye 98%; Hapa utahitajika kuandaa kiasi cha mililita 14.5 za Glycerol 98% ambayo hii waweza ipata famasi ambako huzwa katika ujazo wa mililita 100. 
  • Maji masafi au maji yasiyo na chumvi chumvi (distilled water); Maji yasiyo na chumvi huandaliwa kwa kupooza mvuke utokanao na maji yanayotokota na wakati maji safi huandaliwa kwa kuchemsha maji na kuyapoza. Unaweza pata maji haya kwenye maduka yauzayo kemikali za maabara au katika maduka ya dawa.

Baada ya kuandaa vitu vyote hapo juu, anza kwa kumimina vimiminika hivyo kwenye chombo chenye ujazo wa lita moja kwa kuanzia na Haidrojen peroksaidi, baadae Glycerol, Pombe na mwisho weka maji masafi hadi kwenye alama inayonyesha lita moja au mililita 1000. Kisha tikisa bidhaa yako kwa muda wa dakika tano au chukua kikorogeo kwa ajili ya kuchanganyia. Hapa kikorogeo chetu pendekezwa ni chenye asili ya mbao (mwiko) au plastiki au chuma kisichoshika kutu (Stainless steel). Kumbuka kufunika kifuniko kwa kukaza vizuri ili kuzuia kiambatanishi cha msingi kupotea na upepo (Evaporate).

 

2. Njia ya pili (Formulation II)

Njia hii hutuwezesha kutengeneza kitakasa mikono kiasi cha Lita moja chenye viambata katika wingi huu; Pombe ya Isopropail (Isopropyl alcohol 75%v/v), Haidrojen peroksaidi 0.125v/v, Glisarini 1.45% v/v.

  •     Kemikali iitwayo Haidrojen peroksaidi (H2O2) ya 3%; Hapa utahitajika kuandaa kiasi cha mililita 41.7 za Hydrogen peroxide 3% ambayo hii waweza ipata famasi ambako huzwa katika ujazo wa mililita 100.
  •     Pombe ya aisopropail (Isopropyl alcohol) yenye 99.8%; Hapa utahitajika kuandaa kiasi cha mililita 833.3 za pombe hii yenye asilimia 98.8 ambayo hii pia waweza ipata katika maduka yauzayo kemikali za maabara.
  •      Kemikali iitwayo Glycerol yenye 98%; Hapa utahitajika kuandaa kiasi cha mililita 14.5 za Glycerol 98% ambayo hii waweza ipata famasi ambako huzwa katika ujazo wa mililita 100. 
  •     Maji masafi au maji yasiyo na chumvi chumvi (distilled water); Maji yasiyo na chumvi huandaliwa kwa kupooza mvuke utokanao na maji yanayotokota na wakati maji safi huandaliwa kwa kuchemsha maji na kuyapoza. Unaweza pata maji haya kwenye maduka yauzayo kemikali za maabara au katika maduka ya dawa.

Baada ya kuandaa vitu vyote hapo juu, anza kwa kumimina vimiminika hivyo kwenye chombo chenye ujazo wa lita moja kwa kuanzia na Haidrojen peroksaidi, baadae Glycerol, Pombe na mwisho weka maji masafi hadi kwenye alama inayonyesha lita moja au mililita 1000. Kisha tikisa bidhaa yako kwa muda wa dakika tano au chukua kikorogeo kwa ajili ya kuchanganyia. Hapa kikorogeo chetu pendekezwa ni chenye asili ya mbao (mwiko) au plastiki au chuma kisichoshika kutu (Stainless steel). Kumbuka kufunika kifuniko kwa kukaza vizuri ili kuzuia kiambatanishi cha msingi kupotea na upepo (Evaporate).

 

Matumizi ya kila kiambatanishi.

Kila kiambata katika bidhaa yetu kinayo kazi yake ya msingi ambayo inakamilisha malengo na madhumuni ya kiambata hiki.

  • Haidrojen peroksaidi (H2O2); Katika bidhaa yetu, kemikali hii inakazi ya kutunza dawa (Preservative) ili isiwe na vimelea aina ya spore ambavyo haviwezi kuuawa na pombe pekee yake.
  • Glisarini (Glycerol); Hii huongezwa kwenye bidhaa ili kuifanya bidhaa yetu isichubue mikono yetu tutumiapo na kuipa unyenyevu mikono (Humectant). 
  • Pombe (Ethano au Isopropail); Hii ni pombe kama pombe zingine ambayo katika bidhaa yetu ina kazi ya kuuza vimelea kama Bakteria, Kuvu (fangazi), parasaiti na Baadhi ya virusi. Hiki ndicho kiambata hai ambacho kitaalamu huitwa Active Pharmaceutical Ingridient (API).

Utunzaji wa bidhaa yetu.

Zipo tahadhari kadha wa kadha ambazo tunapaswa kuzifahamu ili kuepuka kusababisha ajari mahali tunapoandalia bidhaa hii au hata kwa mtumiaji. Tahadhari hizi ni Pamoja na zifuatazo;

  • Weka mbali na chanzo moto. Pombe hizi huweza kulipuka kirahisi sana kwenye eneo lolote lililo la Jotoridi la digrii 10. Hivyo inashauriwa kuitunza sehemu yenye ubaridi kama vile kwenye jokofu au friji.
  • Hakikisha kila wakati dawah hii inakua imefunikwa vizuri na kifuniko cha chombo ulichotumia kutunzia. Kutokufanya hivyo husababisha dawa kupotea kirahisi kwenye hew ana kufanya dawa hii kukosa ufanisi na uwezo katika matumizi yake.

Kama una swali au maswali tafhadhari tuachie swali hapo chini na tutakujibu mapema kadri tutakavyopata ujumbe kuwa umeacha swali.

Comments