UFAHAMU UGONJWA WA MARBURG

 UGONJWA WA MARBURG 

Kuwepo kwa ugonjwa huu nchini.

Mnamo tarehe 21 machi mwaka huu (2023), serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, kwa mara ya kwanza ilitangaza mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Virus nchini. Ugonjwa huu ulibainika kuwepo huko wilayani Bukoba Mkoani Kagera, ambako wagonjwa wanane (8) waliokuwa wakihudumia waligundulika kuwa wanamaambukizi ya Ugonjwa wa Unaosababishwa na kirusi kiitwacho Marburg. Katika watu hao wanane, watu watano (5) tayari walitolewa taarifa kuwa wamepoteza Maisha, katika hao waliopoteza maisha, wawili ni watoa huduma za Afya. 

Jitihada zimefanyika na hatua zimechukuliwa kuudhibiti ugonjwa huu hatari wa Marburg Virus na Zaidi ya watu 161 wanahisiwa kuwa wanaweza kuwa wameambukizwa wameshatengwa mahali (karantini) ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu. Pamoja na hayo,serikali imetuma kikosi kazi huko mkoani kagera kuudhibiti ugonjwa huu hatari unaoweza kusababisha kifo haraka sana.

Maelezo machache juu ya kirusi cha Marbug na ugonjwa.

Kirusi cha Marburg ni aina kirusi ambacho kinapatikana kwenye kundi moja na kirusi kinachosababisha Ebola, kundi hili huitwa filoviridae. Kirusi hiki kiligunduliwa kwa mara ya kwanza huko Belgrade – Serbia, Ujeruman sehemu iitwayo Marburg and frankfurt, mnamo mwaka 1967. 

Muonekano wa Kirusi Marburg Mwenye darubini [Chanzo cha Picha ni GETTY IMAGE]

Mlipuko wa ugonjwa huu unahusikwa na ajari iliyojitokeza maabara ya kufanyia tafiti iliyokuwa inatumia sokwe wa kijani (Cercopithecus aethiops) kama viumbe wa majaribio sokwe hao kitaalam wanaitwa waliochukuliwa huko Afrika ya Mashariki nchini Uganda. Hata hivyo kadhia kadhaa zimeripotiwa kutokea huko Nchini DRC (Congo), Kenya, Afrika ya kusini na Angola huku chanzo kikionekana kuwa ni wanyama wa mwituni ikiwemo sokwe na watu waliokutwa na huu ugonjwa walionekana kuwa waliwahi tembelea Uganda huko nyuma. Miongo kadhaa baadae 2008, ugonjwa huu ulipatikana kwa mtalii aliyetembelea pango lililoachwa lenye popo waitwao Rousettus huko Nchini Uganda. 

"What is Marburg virus" around 2...9 and "Ghana Marburg case" 

Picha halo juu inamuonyesha popo jamii ya Rouseteus na Kifaa cha kutunzia sampuli. 

Na wakati huo, ugonjwa huuKirusi Marburg na Kirusi kinachosababisha Ebola, Kwa mujibu ya tafiti, kinauwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90 hii ikiwa na maana kwamba mtu atakaye ambukizwa ugonjwa huu kuna uwezekano wa kupatwa na umauti kwa asilimia 90 na asilimia 10 tu ndio nafasi za kupona. Hata hivyo dalili za ugonjwa huu huanza kuonyesha ishara na dalili zake kwa mtu aliyeathirika ma ugonjwa huu ndani siku 3 had 21 ikitemeana na uwezo wa mwili kukabiliana na maradhi (Kinga ya mwili). 

 

Ni watu gani hasa wako hatarini Zaidi kwenye ugonjwa huu hatari ?

Kwa mujibu wa tafiti, Watu ambao wako kwenye hatari Zaidi kupata matatizo kubwa endapo wataambukizwa/watashambuliwa na ugonjwa huu ni Wanawake wajawazito, sababu ya hili jambo haijajulikana bado japo sababu ya haraka haraka ambayo inaweza kuwa sababu ni kutokana na mabadiliko wayapatao wajawazito ikiwemo na kulemaa kwa kinga ya mwili katika kipindi cha ujauzito. Hata hivyo, watu walio na uwezekano mkubwa kusambaza ugonjwa huu kwa njia ya Kujamiiana ni Wanaume kwani huu ugonjwa hupendelea kuishi kwenye kwenye maji maji ya shahawa za mwanaume.

Je ugonjwa unasambaa kwa njia gani hasa ?

Tukirudi nyuma hapo kwenye historia fupi ya ugonjwa huu, Ugonjwa huu umeonekana kuwa unatoka kwa Wanyama kitaalamu inaitwa Sporadic disease. Ugonjwa huu unaweza kusamba kwa njia ya maji maji ya mwili kutoka kwa mtu ambaye ni mgonjwa. Maji maji hayo ni kama vile Kinyesi cha mtu anayeharisha, Jasho, Mkojo, Shahawa, Maziwa, Kimiminika Kizito kinachomlinda mtoto tumbo (amniotic fluid), Mate, Matapishi  na Damu. Tizama picha hapo chini kwa uelewa Zaidi.

 

Baadhi ya njia ambazo mgonjwa wa MVD huwa nazo.   

Ni nini dalili za ugonjwa huu ?

Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, ugonjwa wa Marburg unazodalili ambazo mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu huonyesha. Dalili hizo ni Pamoja na zifuatazo; 

Kwanza tuanze na dalili ambazo hujitokeza mapema pindi mtu anapoambukizwa kimelea hiki; 

  • Homa kali, 
  • Maumivu makali ya kichwa, 
  • Mwili kujisikia kuumwa,
  • Mwili kukosa nguvu 
  • Maumivu ya misuli,
  • Kukosa hamu ya kula

Kuna zile dalali zinazojitokeza baada siku mbili au tatu ambazo ni; 

  •        Kuharisha maji maji, 
  •        Maumivu ya tumbo, 
  •       Kutokewa na upere mwili mzima, 
  •       Koo kuwasha na 
  •      Macho kuwa mekundu. 

Dalili ambazo hutokea baada siku kuanzia siku ya tano (5) hadi siku ya saba (7) baada ya kuambukizwa ugonjwa huu ni Pamoja nakutokwa na damu puani, mdomoni, masikioni. Tafiti zimeonyesha kuwa vifo vingi hutokea baada ya siku 8 hadi tisa toka dalili za awali zianze kuonekana.

 

Ni makundi gani ya watu yako hatarini kuambukizwa ugonjwa wa MVD ?

Watu ambao wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huu wa marvurg virus ni Pamoja na;

  1. Watu wanaoishi au wamezuru eneo waliopo sokwe na popo waitwao rosetteus kugusana nao au kugusa maji maji yatokayo kwenye miili yao (kama ilivyoorodheshwa pale juu) hawa viumbe.
  2. Watoa huduma za Afya wanaohudumia wagonjwa walio na maambukizi ya vimelea hivi. Watumsihi wa Afya kama; Madaktari, Wauguzi, Wafamasia watoao huduma za kitabibu na wengineo ambao wameshirikwa namna moja au mbili kumhudumia mgonjwa.
  3. Watu wanaohudhuria mazishi ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa huu. Hii ndio sababu serikali huchukua jukumu la kuwazika wapendwa hawa ili kuzuia kuenea au kusambaa kwa ugonjwa huu.

Picha inaonyesha wataalamu wakiwa wamebeba mwili [Picha ni GETTY IMAGE]

Je, kuna dawa au chanjo yoyote dhidi ya ugonjwa huu ?

Kwa mujibu wa Kituo cha kudhibiti magonjwa barani ulaya (Euro CDC), Hakuna dawa ambayo mpaka sasa imethibitishwa kuonyesha uwezo wa kupunguza au kuviua vimelea vya Kirusi cha Marburg. Hivyo matibabu yanayofanyika ni kumsaidia mgonjwa kupona na sio kumuua yule kimelea kwa lugha ya kiingereza wanaita supportive therapy. Matibabu ya kumsaidia mgonjwa kurudia hali nzuri kiafya hujumuisha na Pamoja na kuongezewa maji-dawa yenye madini mbali mbali kama Sodium, Potassium (Rehydration), Kuongezewa damu na bidhaa za damu kama platelets na pia kukabilia na dalili zingine zinazoonekana kwa mgonjwa. Mtu anaweza kuuliza kama kuna chanjo dhidi ya ugonjwa huu, jibu ni kwamba ugonjwa huu hadi sasa haujapatiwa chanjo yoyote. 

Pamoja na hayo, tafiti mbali mbali ulimwenguni zinaendelea kutafuta chanjo ya ugonjwa huu. Ikumbukwe kuwa, mgonjwa anayo nafasi ya kupona mapema kama ataanza matibabau mapema.  iwezekananvyo, hivyo kuchelewa Zaidi hupunguza uwezekano wa mgonjwa kupona au kuimarika kiafya. Kama utamuona mtu yoyote akiwa na dalili zilizotajwa hapo, ni vyema ukatoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za Afya mapema iwezekanavyo ili kuokoa Maisha yake na pia kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu.

 

Jinsi ya kuzuia au kujikinga dhidi ya Ugonjwa huu. 

Ugonjwa huu, kama nilivyoanza kuzungzumzia hapo juu, unaenezwa kujia ya kugusana. Kugusana kimwili na maji maji ya mwili kutoka kwenye mwili wa Mtu aliyeambukizwa na ugonjwa huu. Njia moja wapo ni ; 

  1.  Kuhakikisha hugusi vitu vyovyote ovyo ovyo hasa hasa mahala alipokuwa akiishi, alipozikwa au kulazwa mgonjwa, kwani mdudu huyu anaweza kubaki hai kwa muda siku arobaini kwenye kitu chochote alipodondoshewa.
  2. Nawa mikono na vitakasa mikono vilivyothibishwa mara tu unapokuwa umetoka hospitali au mahali ambapo kuna mtu anashukiwa kuwa anamaambukizi.
  3. Ukijigundua unavzo dalili za ugonjwa huu, tafadhari kimbia mapema kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za Afya ili kuokoa Maisha yako na wengine wanaokuzunguka.
  4.  Fanya au shiriki ngono salama, hii njia hasa hasa itamsaidia mwanamke aliyeolewa na mwanaume ambaye anahistoria ya kuambikizwa ugonjwa huu kutopata maambukizi kwani mdudu huyu hupendelea kukaa kwenye maji maji ya shahawa (semen). Hivyo basi, ni vizuri kutambua kuwa ngono salama inasaidia pia kupunguza uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya dhinaa.


Pamoja na hayo, ugonjwa huu unaweza kuzuilika kwa kuepuka kutembelea maeneo yaliyo au yanayosadikiwa kuwa na mlipuko wa ugonjwa huu. Tahadhari nafuu kuliko Tiba au madhara yenyewe. Usipuuze chukua tahadhari.

 

Comments