Habari gani Ndugu msomaji wa Blog Yetu hii pendwa. Hapa leo nimekuandalia Makala itakayokuelekeza mambo kadha wa kadha kuhusu ujio wa vigezo vipya vya kujiunga na Diploma ya Famasi katika vyuo vya kati vilivyo chini ya Wizara ya Afya na Wizara ya Elimmu Mafunzo na Ufundi kupitia chombo kiitwacho NACTVET (Ambapo mwanzo chombo hiki kilijulikana kama NACTE).
NACTE kama chombo kilichopewa mamlaka ya kusimamia mafunzo ya Ufundi ambayo hutolewa na vyuo vya Kati, Hivi juzi kati kimepitisha vigezo vipya vya kujiunga na Diploma ya Famasi. Vigezo hivi vimeleta minong’ong’o mingi katika katika Tasnia hii ya Mafunzo ya Sayansi za Afya na Afya kwa ujumla. Wadau wengi wamepatwa na msawali maswali mengi juu ya ujio wa Vigezo hivi vipya, na moja ya wadau ambao wameachwa bila majibu ni pamoja na wanafunzi waliokuwa waliomaliza kidato cha nne mwaka Jana ambao walikuwa wanatarajia kujiunga na famasi lakini sasa ndoto yao kusoma famasi kama inafifia.
Ni nani alipitisha vigezo hivi vipya ?? Jibu la hili swali laweza kuwa ni moja ya majibu yanayotafutwa huku na kule kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao isiyo ya kijamii na mtaani pia. Na kusema ukweli, Aliyepitisha vigezo hivi sio mtu mmoja bali watu wengi ambapo walishiriki katika kupitia upya vigezo vya kujkiunga na Stashahada (Diploma) ya famasi. Kama ilivyo kanuni inayoongoza upitishaji wa vigezo vya kujiunga na Diploma ya famasi, Kila baada ya ,miaka mitano vigezo hivi huhitajika kupitiwa vyema kwa kuangalia chungu na Tamu za vigezo hivi katika ubora wa Elimu inayotolewa nchini kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa kiujumla.
Kwenye mchakato huo wa kupitia vigezo vya kujiunga na Diploma ya Famasi, Wadau waliohusishwa katika kupitia na kuandaa vigezo hivi walikuwa kama kutoka Mabaraza/Vyombo vifuatavyo;
- Baraza la mafunzo ya Ufundi (NACTVET)
- Wizara ya Afya (MOH)
- Chama cha Wamiliki wa Vyuo Binafsi Vya Kati Vya Afya (APHECOT)
- Chama cha Wafamasia (PST)
- Baraza la Famasi (PC)
- Wadau wanaohusika na Mafunzo ya Diploma ya Famasi.
- Biolojia (Biology
- Kemia (Chemistry)
- Fisikia (Physics)
- Hisabati (Basic Mathematics) na
- Kingereza (English Language).
Comments