Changamoto ya Kuharisha kwa Watoto wadogo
Watoto wachanga mara nyingi hujisaidia kinyesi laini na tepe tepe kitu ambacho inafanya suala kutambua kama anaharisha au haharishi linakuwa gumu, hii inajitokeza kutokana na chakula walacho wakati huo kinakuwa katika hali ya kimiminika (maziwa ya mama).
Kuharisha ni ugonjwa ambao mtoto hujisaidia kinyezi laini kupitiliza au chenye hali la kimiminika mara tatu au Zaidi kwa siku, halii hii husababisha kupoteza maji na chumvi chumvi pamoja na virutubisho na kumuacha mgonjwa akiwa hana maji na chumvi chumvi za kutosha. Hivyo humuacha mgonjwa akiwa mwili dhaifu au usio na nguvu.
Kwa upande mwingine, kuharisha ni dalili mojawapo ugonjwa wa kuambukizwa yanayosababishwa na wadudu kama bakteria, fangasi na virusi, na magonjwa haya husambaa kwa njia maji machafu (yenye kinyesi) au chakula kisicho salama ikiwemo matunda yanayoliwa bila kuoshwa na vyakula vinapoandaliwa katika mazingira machafu.
Ugonjwa wa kuharisha ni ugonjwa wa pili katika orodha ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo kwa watoto wadogo hasa hasa watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Kwa mujibu wa tafiti za kitabu inakadiliwa kuwa, watoto takribani bilioni 1.7 huugua ugonjwa huu kila mwaka, na katika hao, watoto takribani 525 000 hupoteza maisha. Lakini pia, ugonjwa huu umekuwa ni moja ya sababu kuu za utapiamlo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.
UGONJWA WA KUHARISHA UMEGAWANYWA KWENYE MAKUNDI MAKUU MATATU, NAYO NI;
Mharisho unaoendelea (Persistent diarrhea)
Ni Ile hali ya mtoto kuhara kwa siku kumi na nne (14) au Zaidi. Wadudu wanahusishwa na kusababisha aina hii ya mharisho ni pamoja na E.coli na Amiba
Mharisho sugu (Chronic diarrhea)
Ni ile hali mtoto anahara kwa muda wa siku ishirini na nane (28) au Zaidi. Wadudu wanahusishwa na kusababisha aina hii ya mharisho ni pamoja na E.coli, P.carini na kriptosporidia.
Kuhara damu (dysentery)
Ni ile hali mtoto anahara kinyesi chenye chembe chembe hai za damu, wakati mwingione huita tumbo la kuhara. Wadudu wanahusishwa na kusababisha aina hii ya mharisho ni pamoja na Shigella, Amiba, Kompailobakta na bakteria jamii ya salimonella wasiosabbaisha taifodi.
Dalili za zinazojionyesha kwa mgonjwa aliyepungukiwa maji (dehydrated) kwa sababu ya kuharisha mfululizo ni pamoja na zifuatazo;
- Kutotulia na wakati mwingine anakuwa Analia lia kila mara.
- Mwili wake kukosa nguvu na kulala lala kila wakati (Kuwa mlegevu)
- Macho yanaingia kwa ndani, hii hali lugha ya kiingereza inaitwa *sunken eyes*
- Ngozi ya mtoto pia hupauka
- Na kuwepo kwa hali ya ubaridi kwenye mikono na miguu.
NINI KIFANYIKE KUZUIA MTOTO WAKO ASIPATE TATIZO HILI LA KUHARISHA
- Hakikisha unanawa mikono yako na maji safi yanayotiririka kabla na baada ya kumlisha mwanao
- Hakikisha unanawa mikono yako kwa sabuni na maji safi yanayotiririka kabla na baada ya kumsafisha mtoto baada ya kujisaidia
- Hakikisha unanawa mikono yako kwa sabuni na maji safi yanayotiririka kabla na baada ya baada ya kutoka chooni.
- Tumia maji safi na salama kumnywesha mwanao pindi unapokuwa unampatia maji ya kunywa mtoto.
- Hakikisha unaandaa chakula chako na cha mtoto katika mazingira safi na salama ili kuzuia mambukizi mapya ya wadudu wanaosababisha kuharisha.
NINI CHA KUFANYA UKIMUONA MWANAO NA UKO MBALI HIZO DALILI NA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA;
Kama mtoto ataonekana na hizo dalili zilizotajwa hapo juu na uko mbali unaweza kufanya yafuatayo wakati ukifanya maandalizi ya kwenda kituo chochote cha Afya kilicho karibu nawe;
- Mpatie vyakula vyenye asili ya maji maji kama vile; Supu/Mchuzi wa mboga iliyoandaliwa vizuri, Maji ya mchele, kimiminika cha yogati na maji masafi na salama. Lakini pia Unashauriwa kumpatia maji yenye mchanganyiko wa sukari na chumvi ambayo haya unawezakuyapata kwa kununua unga unga ulioandaliwa tayari au Oro (Lugha ya mtaani) ambayo kitaalamu inaitwa ORS (Oral Rehydrating Solution).
- Mchanganyiko huu husaidia kurudishia maji na chumvi chumvi zilizopotea na pia humpatia nguvu mgonjwa. Tahadhari hakikisha maji unayotumia kuandaa hiyo ORO yawe safi na salamana hii oro unainunua duka la dawa lililokaribu nawe.
- Na baada ya hapo kama utaona mtoto anaendelea kuharisha, na umri wake si chini ya mwaka mmoja Tumia unga wa ngano kidogo ambayo utaichanganya na maji safi kiasi kidogo tu na andaa mchanganyiko Fulani ambayo unafanana na ule wa kuandaa mandazi kisha mpatie. Hii itamsaidia mtoto kuacha kuharisha na hivyo kuzuia hali isiwe mbaya sana. Njia hii haijathibitishwa kitaalam kuwa na manufaa pamoja na kuwa inatumika mara kwa mara kwa watu wazima na watoto wenye umri.
- Baada ya hapo nenda kituo chochote Afya kilicho karibu yako kwajili ya matibabu Zaidi. Kama una swali weka kwenye kisehemu cha maoni nasi tutakujibu mara tu tutakapokutana na swali lako. Ahsanteni sana.
REJEA
- Shah, Mohammed Salman (2011) Home-based management of acute diarrhoeal disease in an urban slum of Aligarh, India. J Infect Dev Ctries 2012; 6(2):137-142.
- Https://www.who.int/publications-detail-redirect/9789241548083
- Https://www.who.int/health-topics/diarrhoea#tab=tab_1
Comments